4/17/2022

Yanga Yakubali Kuishangilia Simba Uwanja wa Mkapa leo Dhidi ya Orlando
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli.
UONGOZI wa Klabu ya Yanga, umesema leo Jumapili utakuwepo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, kwa ajili ya kuisapoti Simba itakapokuwa inacheza dhidi ya Orlando Pirates.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassan Bumbuli wakati Simba leo wakitarajiwa kuwa wenyeji wa Orlando Pirates katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Akizungumza jijini Dar, Bumbuli alisema: “Nitafika Uwanja wa Mkapa Jumapili kwa ajili ya kuisapoti Simba, watani wetu ndiyo wawakilishi wa nchi pekee kwa sasa.

“Tunatamani kuona japo timu moja inachukua kikombe cha CAF ili timu za Tanzania ziwe zinaogopwa na kuheshimiwa. Tukienda nje hata wapinzani watuogope, hivyo watakuwa wakicheza kwa uoga.


 
“Hata wale Al Ahly, pale kwao Cairo, huwa wanazifunga baadhi ya timu kutokana na uoga.”

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger