4/15/2022

Yanga yalainishiwa Ubingwa BaraYANGA ishindwe yenyewe tu sasa, baada ya Bodiya Ligi kufanya mabadiliko madogo ya ratiba ya Ligi Kuu na kuurudisha nyuma mchezo wao na Namungo na sasa utapigwa Aprili 23, wiki moja kabla ya kuvaana na watani wao Simba.

Awali mechi hiyo ilikuwa haijapangiwa tarehe, lakini jana Bodi ya Ligi kupitia Ofisa Habari, Karim Boimanda ilisema sasa itapigwa Jumamosi wiki ijayo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga ikiwa wenyeji.

“Sio kama Yanga imeomba, ila ukweli ni kwamba ni mechi zilizokuwa hazijapangiwa tarehe sambamba na mechi ya Azam na KMC ambayo sasa itapigwa Mei 7, huku ile ya Biashara United na Dodoma Jiji utapigwa Mei 5,” alisema Boimanda.

Upande wa Yanga kupitia akaunti zao za mitandao ya kijamii waliweka ratiba ya mechi hiyo, ikiwa ni kama nafuu kwao kwani haikuwa na mechi ya mashindano tangu ilipocheza robo fainali ya Kombe la ASFC dhidi ya Geita Gold.

Yanga ilikuwa na siku 20 za kujiandaa na pambano lao na Simba litakalopigwa Aprili 30, lakini kupangwa kwa mchezo wa Namungo ni kama imerahisishiwa kazi katika kuzipunguza mechi ngumu ikisaka ubingwa wake wa 28 wa Ligi Kuu Bara. Yanga yenye pointi 51 baada ya mechi 19 kama Yanga itashinda mechi hiyo ya Namungo itajirahisishia harakati zake za ubingwa, kabla ya kuvaana na Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi zao 41.

Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage alikaririwa hivi karibuni kwamba Simba ilikuwa na kizingiti cha ubingwa katika mechi kama tano ikiwamo ya KMC na Azam (ambazo zote Yanga imeshinda), Simba, Namungo na Mbeya City.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger