5/06/2022

Agoma Kutoka Jela Baada ya Kuachiwa Huru

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPAKiongozi wa dini ya Kiislamu ameiomba mahakama ya Kenya kutomwachilia huru licha ya kuachiliwa kwa makosa ya ugaidi.

Sheikh Guyo Gorsa Buru alikamatwa Januari 2018 kaskazini mwa Kenya na kushtakiwa kwa kuwa na nyenzo za kulitangaza kundi la kigaidi na kwa kushirikiana na kundi la wanamgambo wa al-Shabab.

Lakini wiki hii, mahakama ilimwachilia ikisema kuwa serikali imeshindwa kuthibitisha kesi yake.

Hata hivyo alikataa kuondoka katika gereza maarufu la Kamiti akisema anahofia maisha yake huku akidai kuwa anaweza kutekwa nyara na kuuawa na serikali mara tu atakapokuwa huru.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger