5/08/2022

Ahmed Ally aomba radhi kwa kusema vilabu dhaifuHatimaye Afisa Habari wa Klabu ya soka ya Simba, Ahmed Ally amejitokeza na kuomba radhi kupitia mitandao yake ya kijamii kufuatia hivi karibuni kuibua mjadala kwa kusema kuwa timu nyingi za Ligi Kuu msimu huu ni dhaifu kuliko msimu uliopita.
Nimefarijika kuona agenda niliyoanzisha imejadiliwa kwa siku tatu,kuweka kumbukumbu sawa hakuna mahala nimesema tuna LIGI DHAIFU, nimesema timu nyingi msimu huu zimekuwa dhaifu kulinganisha na msimu uliopita,metoa hoja nilizoona sahihi na walipinga wanetoa hoja zao sahihi.

Nilichofurahi ni kuona watu wamejadili kwa kutumia facts japo kama kawa wengine wameropoka hao hawawezi kubadilika kwa sababu wa uwezo wao ni mdogo.

Imewalazimu watu kufukua misimamo ya Ligi nyingine kulinganisha na hapa kwetu, yote ni kutetea hoja zao.

Imewalazimu watu kuhesabu magoli na points za msimu uliopita, hiyo ni kutetea hoja zao, hii ndio mijadala tunayoitaka kwenye mpira wetu sio mjadala wa maisha binafsi, tunataka mijadala ya kimpira sio vichambo.

Sisi watu wa media ndio wenye jukumu la kuanzisha mijadala yenye tija(AGENDA SETTING).

Niwatake radhi wale wote nilio wakwaza kwa kusema timu nyingi DHAIFU , na mimi nikiri kua ni kweli msimu huu kwenye Ligi yetu kuna ushindani lakini hawa 14 wanashindania nini? Jibu baki nalo mwenyewe.''Ahmed Ally

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger