Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Dodoma Jiji vs Yanga Mechi ya Leo"
1: WHAT A WIN ✊ POINTI 3 MUHIMU KATIKATI YA PRESHA KUBWA. WELL DONE WANANCHI👏 Vile ndio timu yenye dhamira ya Ubingwa inatakiwa kurejea baada ya nyakati ngumu

2: ILE 'PITCH' ya Jamhuri ni AIBU! 'Standard' ya Game inapotea kwa pitch kukosa viwango. Nawaza, Rais Samia alipotoa agizo la VIWANJA ni watu hawakuelewa au ni kusudi tu? Kuna jambo la haraka inabidi kufanyika pale

3: 'FIGHTING SPIRIT' ya wachezaji wa Yanga ilitosha kueleza kilichokuwa kwenye vichwa vyao. Walikimbia kilomita nyingi sana.. walipambana kushinda 'Second Balls' nyingi! Kubwa zaidi walilobadili leo, YANGA KWANZA, MAYELE BAADAE.

4: 'Tactically' Kocha wa Dodoma Jiji ni kama alijiandaa kudili na Ufundi wa Yanga katikati ya uwanja Lakini bahati mbaya kwake, Yanga wakaja tofauti? Kivipi?

5: Nabi akarusha karata tofauti. Kutokana na changamoto ya Pitch, akaweka wachezaji sahihi katika kiwanja kile. Akaiacha akili ya Bangala na Aucho akaja na mpango wa kutegemea mapafu ya kina Mauya na Ambundo

6: Yanga wakaupeleka mchezo pembeni kwa kasi kubwa. Moloko na Ambundo wakawa kwenye kiwango chao bora. Mauya akawa Form pia kwenye kuutembeza mpira kwa kasi. Kuna jambo Yanga wamejifunza pia kwenye lile bao la kwanza! Lipi?

7: Pasi ya Moloko kwenda kwa Ambundo ni matokeo ya Yanga kujua faida ya kutumia Movement za Mayele uwanjani. Huwezi kuzuia Mabeki kumkamia Mayele lakini unaweza kuwaadhibu kiufundi kwa mikimbio ya kutokea pembeni

8: Emmanuel Martin.. Mchezaji wa mechi kutoka kikosi cha Dodoma Jiji..👏 Alivyorudi kucheza chini ni kama uimara wake ukaongezeka. Akawa mzuri kwrnyr kukaba na kushambulia

9: Diarra🙌 WHAT A PERFOMANCE. SAVE MBILI BORA SANA ZA MECHI. Ziko nyakati ubora wa kipa unaweza kuisaidia Timu kushinda mechi kwa kufanya Saves za kukata presha ya wapinzani

10: Bao la 2 la Yanga ni OFFSIDE. Kama Shuti la Mauya lingekwenda moja kwa moja, hakuna tatizo. lakini kipa kuucheza, tunarudi kutazama kuangalia nafasi ya Ambundo na Mayele wakati Mauya anapiga mpira. Walikuwa eneo la kuotea na waliuingia mchezo! Sijaelewa kwanini FRANK KOMBA alinyoosha na kushusha kibendera kwenye Tukio lile

Nb: 'YANGA A' 2-0 'YANGA B' 😃
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad