5/04/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona RUVU vs YANGA Leo"

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPA
1: MECHI YA KIUME✊ Sio kwamba RUVU waliikamia Yanga.. RUVU wako kwenye nafasi mbaya kwenye msimamo. Iliwalazimu kuvuja jasho jingi kuokota alama moja ya Thamani mbele ya Yanga. WAMEPAMBANA MNO👏

2: Cedric Kaze ni kama alichelewa mno kuielewa Pitch ya Lake Tanganyika. Nafikiri Option ya kucheza na 'Dabo Straika' kwenye 4-1-3-2 ungekuwa mpango sahihi kucheza kwa mipira mirefu iliyokuwa inaingia kwenye boksi la Ruvu Shooting

3: Well Done Mzee Mkwasa👏 Akili kubwa kwenye mpango wa mechi, uchaguzi wa wachezaji [Abrahaman Mussa kurudi kwenye nafasi ya ulinzi wa kulia, Chilambo kwenda kushoto] ilikiwa kete muhimu sana ya kupunguza madhara ya Yanga pembeni

4: Jezi namba 6 mgongoni.. ALLY MUSA KOMBO🙌 Kifua chake kilijaa upepo wa kutosha kukimbizana na movement za viungo wa Yanga.. Alikata sana umeme! Lakini alistahidi kadi nyekundu kwa kumkanyaga Dickson Job

5: Mayele hajapata bao ila ukiendelea kubeza uwezo wake bila/akiwa na mpira utakuwa hujui kitu kuhusu Football. Ni straika mpambanaji sana. Anampa sababu shabiki jukwaani kuamini bao linatafutwa. Mohammed Makaka anaweza kuibusu milingoni ya lango lake kumpa 'Clean Sheet' mbele ya Mayele

6: Nilipenda ile 'Chemistry' ya Aucho na Sure Boy katikati ya Uwanja. Ni 'Pivot' iliyokuwa na hesabu nzuri kwenye hatua zao kuvamia eneo la juu.. Kazi nzuri ya Kombo ndio iliwapunguza madhara kwrnye kumalizia lakini 'Build Up' yao ilikuwa Super sana

7: Rashid Juma kaharibu mechi yake kwa 'utoto'. Alimpa mechi nzuri sana Shomari Kibwana. Kinywa chake kimefanya wengi wasahau Dribbling yake, kasi na uwezo wake wa kutunza mpira

8: Kuna vita ilikuwepo kati ya Dickson Job na Sadat Nanguo🙌 Sadat alimjaribu Dick kwenye kasi, nguvu na Dick alimpa majibu mazuri kila wakati..

9: Lile ni BAO HALALI. SADAT NANGUO HAKUWA ENEO LA KUOTEA. Line 1 Changwalu na alisimama kwenye eneo sahihi kabisa Lakini alishindwa kutafsiri vyema sheria

10: Chilambo 👏 Bangala 👏 Saido na Feisal mechi iliwakataa. AbdulSwamad Kassim akibaki kwenye Form ile ni one of the best DM kwenye jezi ya Ruvu

Nb: 'Panya Road' wanaocheza mpira 😃
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger