Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Simba Ikiichapa Kagera Sugar, Gap Point 8"

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
1: POINTI 3 MUHIMU! It's Not Over Until It's Over.. Kauli mbiu ya Kila shabiki wa SIMBA SC kwa sasa. 'Gap' ni Pointi 8 .. Presha imeongezeka kwenye mbio za Ubingwa! Lolote Linaweza kutokea kwenye FOOTBALL

2: Well Done Pablo👏 Nimeenjoy kutazama matumizi ya 'Half Spaces' Simba walipokuwa wanashambulia.. Zile pasi, Ile mikimbio ni kitu kinachoanzia kujengwa katika uwanja wa mazoezi..

3: Kocha wa Kagera Sugar, Baraza alikuwa na mpango mzuri wa kutega shambulizi lake kwenye Quick Transition.. Lakini 'Quality' ya wachezaji wake wanapofika kwenye 'Final Third' ya Simba ndio iliwagharimu. Walitupa mipira mingi kwa 'Shots' zisizokuwa na Target

4: Kuna raha Henock akicheza kama Beki wa kati.. Lakini kuna Raha zaidi kumuona kama Kiungo mkabaji. What A Player! Uwezo wake wa kupiga pasi, kupandisha timu uliwapa wakati mgumu viungo wa Kagera

5: MUZAMIR ✊ WHAT A PLAYER! Tusisubiri akosee tuweke Points zetu. Jamaa yuko kwenye kiwango bora sana. Jinsi anavyolink timu kutoka chini kuja juu..🙌 Jambo bora kwake, Uwezo wake wa kupiga pasi za mbele umeongezeka sana👏

6: DICKSON MHILU.. WHAT A PERFOMANCE👏 Alicheza mechi yake kwa kujiamini sana. Alihimili vishindo vya mawinga wa Simba na kuwalazimisha wamkabe.. Jambo pekee analotakiwa kuliboresha ni mpira wake wa mwisho anapokata mstari wa katikati

7: RALLY BWALYA🙌 Football imetawaliwa na namba. Na kwa Assist 2 za viwango ni ngumu kuliondoa jina la Bwalya unapomtafuta Man Of The Match.. What A Player.. Alikuwa kwenye kiwango bora sana cha kuusoma mchezo na kuja na majibu

8: WAWA AMERUDI. Ni kama mwili wake umeshapoa na umerudi tena kwenye mapambano✊ Timing yake kwenye kuhesabu hatua za washambuliaji ni silaha inayopunguza madhara makubwa kwenye safu ya ulinzi ya Simba

9: Well Done John Bocco.. Bao la pili mfululizo👏 Ni nyakati hizi kila shabiki wa Simba anaenjoy kuona Bocco na Kibu wanafunga mfululizo baada ya kupitia kipindi kigumu

10: Yule kiungo wa chini wa Kagera, Appolinaire anajua sana. Hana papara. Anakaba na kusambaza pasi sahihi akiwa kwenye presha..🙌 Bado Kagera wana changamoto kwenye idara ya Golikipa

Nb: Vipi.. Kileleni Baridi bado Lipo au Joto limeanza? 😃

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad