5/09/2022

Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Simba Vs Ruvu Shooting Mtu Akupigwa 4G"1: MNARA UMESOMA! 4G✊ USHINDI WA KIKUBWA. Ile ndio namna nzuri kwa Mnyama 🦁 kurejesha Furaha kwa mashabiki baada ya Dakika 270 za Ligi bila Ushindi

2: WHAT A MOMENT kwa Captain John Bocco✊ Baada ya Siku 295 anafunga bao lake la kwanza kwenye Ligi. Kuna makosa kwa Makaka Lakini ile Shooting ya Bocco ni ya viwango vikubwa sana

3: SAYANSI YA MPIRA. Ni rahisi kulisema hili neno Lakini ni ngumu kulielewa. Watazame Ruvu Shooting. Wanajua nafasi yao kwenye msimamo. Wanajua ratiba yao, Dakika 180 dhidi ya Simba vs Yanga.. Ni nani alitoa wazo la kuipeleka mechi ya Yanga Kigoma?

4: Hela? Labda.. Lakini zina gharama kubwa kiufundi. Haya mabao 4, zimeifanya GOAL DIFFERENCE kuwa 11. Kwa jinsi ushindani wa msimamo ulivyo haya mabao yanaweza kuwa na gharama kubwa kwao mwishoni

5: Well Done Simba👏 Presha ilikuwa kubwa sana kwao kushinda hii mechi. Walitawala sana mchezo. Walitengeneza sana nafasi Lakini iliwalizimu wasubiri kipindi cha pili, Intensity Level ya Ruvu iliposhuka, ndio wakawa watulivu kutumia nafasi zao

6: MUZAMIR YASSIN pale Chini✊ Ni ngumu kuona impact yake kwa jicho la kawaida Lakini aliporudi kwenye eneo la Mkude, uwezo wa pasi, kusukuma timu juu na kuzima pasi za haraka za Ruvu iliwafanya viungo wa juu kuwa huru zaidi kuishambulia Ruvu

7: Zilikuwa Dakika 45 nzuri kwa Nathaniel Chilambo👏 Lakini kipindi cha pili ilifika wakati akashika kiuno na kuinama. Mwili ulikataa kabisa kuendana na kasi ya mchezo

8: Mechi nzuri Bwalya. Bao zuri pia. Nafikiri kama kuna kitu anatakiwa kukifanyia kazi zaidi kwenye uwanja wa mazoezi ni usahihi wa mashuti yake langoni. Ile ndio silaha pekee inayomtofautisha na viungo wengine wa Simba

9: Kibu Dennis.. ✊ Striker Force. Anakupa jasho lake lote kiwanjani kwa ajili ya jezi ya Simba. Anapigwa buti anaamka na tabasamu anasonga mbele zaidi. Bila shaka Yahya Jaffary anabaki kuwa mtu pekee anayeweza kukuhadithia ubora wa Kibu katika mchezo wa Leo

10: Manula ataondoka akiwa mnyonge moyoni. Kwa Golikipa, baada ya umiliki ule wa mchezo kwa Timu, Ushindi mkubwa vile, zawadi pekee unayohitaji ni CLEAN SHEET

Nb: Kwa Pira Lile, Ile nafasi ya 2 hawana mpinzani.. 😃

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger