Aliyetumia gari la serikali kubeba dawa za kulevya asimamishwa kazi

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA
HALMASHAURI ya Jiji la Arusha,imemsimamisha kazi dereva wake, Athuman Magio, kutokana na tuhuma za kutumia gari la halmashauri hiyo kusafirishia dawa za kulevya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji hilo, Dk. John Pima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji hilo, Dk. John Pima, amesema leo kuwa, uamuzi huo uliridhiwa na kamati maalumu ya iliyojadili nidhamu ya mtumishi huyo.

Dk.Pima, amesema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Sikukuu ya Eid El Fitri, Mei 2 mwaka huu.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa na Jeshi la Polisi katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, akisafirisha dawa za kulevya.

Amesema siku ya tukio dereva huyo, akiendesha gari  aina ya Toyota Landcruiser  yenye namba za usajili STJ 7333, majira ya asubuhi, wakati akiwa ametumwa kwenda Wilaya ya  Karatu, kuwachukua maofisa  wa halmashauri hiyo, waliokuwa wilayani humo kwa shughuli za kikazi.

"Aliporudi Arusha, aliegesha gari hilo kwenye ofisi za Jiji na kulikabidhi kwa walinzi kwa kuliandikisha kwenye kitabu cha walinzi,"amesema.

Ameeleza ilipofika jioni alirudi kuchukua gari hilo na kuwadanganya walinzi  alikuwa akiendelea na kazi, hivyo walinzi walimruhusu na kuondoka na gari hilo hadi Wilaya ya Rombo alikokamatwa na Polisi waliokuwa doria.

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPA


 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad