Ambulance yazua kizaazaa, Namungo vs Mbeya KwanzaMCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Namungo na Mbeya Kwanza uliokuwa upigwe kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi umeahirishwa baada ya kuchelewa kwa gari la kubebea wagonjwa ‘Ambulance’.

Mchezo huo uliokuwa uanze saa 10:00 jioni ilitokea sintofahamu baada ya wachezaji wa timu zote mbili kuwa uwanjani pamoja na marefa lakini mwamuzi hakupuliza kipenga kuashiria kuanza kutokana na kutokuwepo kwa Ambulance ambayo ipo kwenye kanuni na taratibu za mchezo.

Mawasiliano ya pande zote mbili yalifanyika na saa 10:24 ambulance iliingia Uwanjani hapo lakini mechi haikuendelea na ilipofika saa 10:35 waamuzi waliingia katikati ya Uwanja kisha kutoka na kuelekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Baada ya hapo timu ya Mbeya Kwanza ikiongozwa na kocha wake, Mohamed Makata na baadhi ya wachezaji nao waliondoka uwanjani hapo huku wengine wakibaki wakipiga stori na wale wa Namungo.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad