5/04/2022

Askari Magereza na Mfungwa Waliokuwa na Mahusiano WametorokaMfungwa aliyetoroka na askari jela anayedaiwa kumsaidia walikuwa na uhusiano maalum , wanasema wachunguzi.

Tangazo hilo kutoka afisi ya mkuu wa polisi katika jimbo la Alabama linasema kwamba ugunduzi huo ulitajwa na wenzake mfungwa huyo Casey White , ambaye ni mshukiwa wa mauaji.

Msako wa kumtafuta mfungwa huyo mwenye umri wa miaka 38 pamoja na askari jela Vickey White mwenye umri wa miaka 56 unaendelea.

Wawili hao walitoroka wakati alipokuwa akimpeleka katika kituo bandia cha ukaguzi wa akili. Maafisa hatahivyo hawajathibitisha iwapo uhusiano huo ulikuwa wa kimapenzi.


Siku ya Ijumaa, siku ambayo wawili hao walitoroka – ilikuwa siku ya mwisho ya kazi . Alikuwa ameiuza nyumba yake na kuwaambia wenzake kwamba alikuwa anapanga kuishi maisha yake katika ufuo wa bahari.

Maafisa wa polisi sasa wanaamini kwamba askari jela huyo alihusika katika kupanga kumtorosha mfungwa huyo baada ya kukiuka itifaki ya jela hiyo na kumsindikiza Casey akiwa pekee.

Wachunguzi walipokea habari kutoka kwa wafungwa wengine katika kituo cha Lauderdale Countywikendi iliopita kwamba kulikuwa na uhusiano maalum kati ya Mkurugenzi White na mfungwa Casey White, Afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo Rick Singleton alisema katika taarifa.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger