Ticker

6/recent/ticker-posts

Askofu Gwajima kutatua tatizo lililodumu zaidi ya miaka 20Mbunge wa Kawe Askofu Josephat Gwajima, amesema hataki kuwa kama wabunge waliopita ambao walishindwa kutatua changamoto ya mtaro wa kupitisha maji ili kuzuia mafuriko ya mara kwa mara iliyodumu kwa zaidi ya miaka 20 katika eneo la Kunduchi Pwani.
Ametoa kauli hiyo baada ya kufanya mikutano yake na wananchi wa Kunduchi Pwani, Tegeta, na Mbweni teta maeneo ambayo yamekuwa na changamoto ya mafuriko kila mara mvua inaponyesha.

Amesema atatoa fedha zake binafsi Ili kuanza kwa ujenzi huo mara moja bila kuwasubiri TARURA waje waanze kujenga kwa kuwa kama atawasubiria basi ujenzi huo utachelewa kuanza na wananchi wataendelea kupata shida.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments