Ticker

6/recent/ticker-posts

Babu Tale Afunguka Wimbo wa Mtasubiri Kufungwa "Dhamira ya Kudumaza Ukuaji na Kujituma"

 Habari Kama Hizi Zinapatikana UDAKU SPECIAL App, Download HAPA Bure: Link here>>>


Kutoka Kwenye Ukurasa wa Instagram Wa Babutale Anaadika Ujumbe Huu Baada Ya Wimbo wa Diamond Platnumz Ft Zuchu Mtasubiri Kufungiwa

"BABA NA MWANA.

Hakuna Mwanadamu anayependa kuchoka anapokuwa katika jambo linalotumia nguvu na akili.

Lakini unaweza kudhani kila jambo ni rahisi pale unapoyaona matokeo ya ufanisi ambao Mtu hajalalamika kuwa mgumu kuutekeleza.

Ebu tazama ugumu wa kufikiri jambo unalodhani mwingine hajawahi kufikiri na likafanikiwa kubeba heshima ya kuwa ni jambo la kipekee?

Kwa kawaida Watu hawatafuti makosa kwenye jambo dogo, bali lile lililokubwa zaidi.

Lakini kabla ya kuamua juu ya jambo kubwa naamini ni muhimu kuhesabu, muda, nguvu, rasilimali na mkanganyiko wa kuliamulia jambo kubwa.

Kiukweli adhabu zinazotolewa na Wazazi kwa Watoto zinatafsiri dhamira ya kudumaza ukuaji, kujituma na kujitegemea.

Si jambo linaloshangaza Mtoto kukimbia shughuli za Familia, kwakuwa utambulisho hauna faida kama adhabu ya ndani inamzidi kibaka aliyeiba kwa kupitia dirishani. #malengo #theblackgodfather" - Babu Tale

HABARI HIZI ZINAPATIKANA  KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO BURE

________________________________

 Join AJIRA YAKO Group for Daily Job Updates CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments