Bandari Dar Kuvunja Rekodi Nyingine..Kupokea Meli Kubwa Nyingine Mei 9

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Siku 30 baada ya Bandari ya Dar es Salaam kuandika rekodi ya kupokea meli yenye mzigo mkubwa zaidi wa magari, rekodi hiyo inatarajiwa kuvunjwa tena Mei 9, 2022 kufuatia ujio wa meli yenye mzigo mkubwa zaidi wa magari.


Akizungumzia hilo Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Nicodemus Mushi amesema meli hiyo iitwayo Meridian Ace inatoka Japan itawasili Dar es Salaam ikiwa na shehena ya magari 4397 idadi ambayo haijawahi kufikiwa kwa mara moja.



Amesema rekodi ya mwisho ilikuwa magari 4041 yaliyowasili Aprili 8, 2022 iliyopokelewa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.



Mushi amesema mafanikio hayo ni matokeo ya kazi ya kutangaza uwezo wa bandari ya Tanzania, inayofanywa na Serikali duniani.



Amesema uwekezaji mkubwa umefanywa na Serikali katika kuwezesha vitendea kazi na maboresho ya miundombinu sambamba na kampeni za masoko na ushirikiano thabiti wa TPA, wateja na wadau wake wengine.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad