Ticker

6/recent/ticker-posts

Bernard Morrison aanika ukweli Simba SC

 


Dakika chache baada ya Uongozi wa Simba SC kutangaza hadharani kumpa mapumziko hadi mwishoni mwa msimu huu, Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison ameibuka na tamko lake.


Simba SC imethibitisha kumpa mapumziko hayo Morrison kupitia taarifa maalum iliyowekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ya MSimbazi leo Ijumaa (Mei 13).


Kiungo huyo aliyejiunga na Simba SC mwanzoni mwa msimu ulipita akitokea Young Africans, naye ametumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuweka wazi kuhusu safari yake ya kuondoka Simba SC, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo.


Morrison ameandika:Nina moyo mzito kutangaza kwamba sitakuwepo kwa muda uliosalia wa msimu huu kwa sababu ya masuala ya kifamilia ambayo ni nje ya uwezo wangu, na huenda yakaathiri utendaji wangu wa kazi ikiwa nitaendelea kuitumikia klabu.


Mengi yanahitajika kusemwa kuhusu hilo lakini naitakia klabu kila la kheri katika michezo yetu iliyosalia. Natumai na ninaomba nitatue hili haraka iwezekanavyo ili nijiunge na timu tena.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments