5/02/2022

Bien Sol:Eric Omondi, ‘Anakera’ Harmonize angemchapa zaidiMwimbaji mahiri wa kundi la Sauti Sol Bien Aime Baraza amemgeuzia kibao mchekeshaji Eric Omondi baada ya kupigwa ngumi na Harmonize na kuthubutu kusema kuwa alitakiwa kuchapwa zaidi.


Katika sehemu ya maoni (comment) ya chapisho la Eric Omondi, Bien alihoji kwa nini kila mtu alikuwa akimshtumu Eric Omondi kwamba ni mtu mwenye maudhi.


“Wewe kwanini kila mtu anataka kukuchapa, Unakera sana. Natamani angekupiga zaidi na ningekua hapo ningekuongezea,” Bien ali-comment.


Maoni hayo yanakuja baada ya ‘ugomvi’ wa muda mrefu wa Bien Sol na mchekeshaji Omondi ambao mara kadhaa wamekuwa wakirumbana mitandaoni.


Hata hivyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram Eric aliweka wazi kuwa walisuluhisha changamoto iliyopelekea kukosekana kwa maelewano baina yao na baadae walionekana kusafiri pamoja hadi Mombasa kwa ajili ya onyesho lililofuata.


“Kama kaka mkubwa, kama host na kama msanii mwenzangu wa Afrika Mashariki nataka kuomba msamaha kwa yote yaliyotokea,” Eric alisema.


Kwa upande wa Harmonize alisema hakuna aliyekamilika na kuongeza kuwa anachukulia kilichotokea kama sehemu ya changamoto za kazi na si vinginevyo.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger