Bobi Wine Amtapikia Nyongo Mwanawe Museveni kwa Kumuita Kaka
Bobi Wine(kushoto) alikerwa na mwanawe Museveni(kulia) kwa kumuita kaka. Picha: Bobi Wine/ Getty Images.
Mchoro huo wa katuni ulikuwa unamuashiria kiongozi wa upinzani Bobi Wine akisema:

"Kiatu hiki ni saizi yangu-usikaribie."

Kisha katuni ya pili ambayo inamuashiria mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ilijibu katika mchoro huo ikisema: "Tulia Kaka! Sio kosa langu, ipo kwenye jeni yangu."

Katuni ambayo hutumika kama sanaa ya maigizo ya maisha ya kweli, ilikuwa ikionyesha wahusika wakijadiliana ni nani atatoshea kwenye kiatu cha Museveni ambaye ameongoza Uganda kwa muda mrefu.


 
Mchoro huo wa katuni ulishirikishwa kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumatano, Mei 18, na mwanawe rais Museveni, Jenerali Kainerugaba ambapo alimtaja Wine kama kaka yake.

"Mimi na kaka yangu mdogo Kabobi tukibishana kuhusu nani anaweza kujaza viatu vya baba yangu! Asante msanii bora nchini Uganda...Kintu!"

Lakini Bobi Wine alionekana kukerwa na jenerali huyo kumuita kaka akisema:


"Mimi si kaka yako na sishindanii viatu vya baba yako. Una haki ya viatu vya M7, ng'ombe na hata kofia yake. Kosa moja unalofanya ni kufikiria kuwa Uganda ni moja ya mali za baba yako ili urithi."

Mwanawe Museveni ashtakiwa kwa kutangaza azma yake ya urais
Tuko.co.ke iliripotia awali kuwa mwanawe Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ametakiwa kujibu shtaka analotuhumiwa la kutangaza nia yake ya kuwania urais nchini humo akiwa bado anahudumu katika jeshi la nchi hiyo.

Katika kesi iliyowasilishwa kwa Mahakama ya kikatiba ya Uganda na Wakili wa haki za binadamu Gawaya Tegulle, aliiomba mahakama hiyo iliyoko mjini mkuu, Kampala, kumzuia Jenerali Kainerugaba kufanya shughuli za kisiasa akiwa bado anatumikia jeshi.

Gideon Moi: Mwenyekiti wa Kanu Kuwania Useneta Tena Baringo
Gawaya pia anataka jenerali huyo ashtakiwe kwa uhaini kufuatia madai dhidi yake ya kupanga njama ya kumrithi baba yake akitumia mbinu "haramu".


 
Kupandishwa kwake vyeo haraka, kuliibua fununu kwamba anaandaliwa kuwa mrithi wa Museveni ambaye ametawala Uganda kwa zaidi ya miaka 30.

Hata hivyo, Rais Museveni mwaka wa 2013 alijitokeza kukanusha madai hayo akisema Uganda sio nchi ya kifalme ambao uongozi unarithishwa kutoka kwa baba kwenda kwa mtoto.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad