BREAKING NEWS: Spika asubiri uamuzi wa mahakama wabunge 19 waliofukuzwa Chadema

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema anasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu wabunge 19 wa Viti Maalum waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Dk Tulia amesema hay oleo Jumatatu Mei 16, 2022 wakati akitoa maelezo ya wabunge hao ambao walivuliwa uanachama na Chadema.

Katika maelezo yake, Dk Tulia amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa wabunge hao kuwa tayari wameshafungua kesi  Mahakama Kuu ya kupinga mwenendo wa kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu na baadaye Baraza Kuu kukataa rufaa yao.

Alhamisi iliyopita kikao cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya kinidhamu kutupilia mbali rufaa ya wabunge hao kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama Novemba 27, 2020.


 
Kikao hicho cha Baraza Kuu la Chadema kilichofanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam, wajumbe walipopiga kura nyingi za kubariki kufukuzwa kwao.

Hata hivyo, baada ya uamuzi huo, licha ya kutarajiwa na wanachama wengi wa Chadema, haukutarajiwa na wabunge hao na Halima Mdee, kiongozi wa wabunge hao na aliyekuwa mwenyekiti wa Bawacha alisema:

“Kilichofanyika pale ni uhuni wa kiwango cha hatari. Hata Mbowe mwenyewe anajua.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad