5/26/2022

Chama Arudishwa Dar, Yanga Washangilia

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


KIUNGO mshambuliaji wa kikosi cha Simba Clatous Chama hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachowakabili Yanga Jumamosi kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza baada ya jana kuondoka kambini.

Inaelezwa Chama alienda Mwanza lakini hakuwa fiti baada ya kupata majeraha siku kadhaa zilizopita huku akiruhusiwa kurejea Dar es Salaam jana.

Baada ya Simba kutua Mwanza Chama alianza mazoezi na wenzake lakini juzi alipelekwa hospitali ya Bugando kwa uchunguzi zaidi na kubaini anahitajika matibabu zaidi.

Mbali na kurejea Dar es Salaam nyota huyo amepewa ruhusa ya kwenda nchini kwao Zambia kushiriki mwaka mmoja wa kifo cha marehemu mke wake aliyefariki dunia Mei 28 mwaka jana.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger