5/18/2022

Chris Brown athibitisha Wizkid kuwepo kwenye album yake ya ‘BREEZY’

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Moja ya wasanii kutoka Afrika mbao nyota zao zimekuwa ziking’ara sana duniani huwezi kuacha kumtaja Ayodeji Ibrahim Balogun BIG WIZZY alimaarufu kama @wizkidayo kutoka nchini Nigeria.

Nyota huyo ambaye anatamba na album ya MADE IN LAGOS ikiwa na ngoma kali kama Essnce anaendelea kugonga vichwa vya habari duniani na hii ni baada ya Nyota wa muziki wa Pop na RnB kutoka Marekani Christopher Maurice Brown alimaarufu kama Chris Brown kuweka wazi kwamba Wizkid ni mmoja ya wasnaii ambao watakuwepo kwenye Album yake mpya “Breezy”


Album hiyo inatarajiwa kutoka Juni 24 mwaka huu na jina la Wizkid ndio jina la kwanza kutokea kwenye orodha ya wasanii 11 ambao Chris Brown amewatambulisha kupitia Insta Story yake, pamoja na kuitambulisha cover la album hiyo.Orodha ya wanamuziki walioshirikishwa kwenye album ya “Breezy” ni pamoja na Wizkid, Ella Mai, H.E.R., Lil Wayne, Blxst, Anderson .Paak, Jack Harlow, Tory Lanez na wengine ambao bado hajawataja.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger