Ticker

6/recent/ticker-posts

Dkt Abbas Ataja Manufaa Ziara ya Rais Marekani

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, Dkt Hassan Abbas amesema kuwa wawekezaji wakubwa zaidi ya watano wameahidi kuja Tanzania baada ya kukutana na Rais Samia nchini Marekani.


Dkt Abbasi ametoa kauli hiyo leo katika mjadala uliokuwa unaendeshwa mtandaoni (Zoom) kuhusu filamu ya Royal Tour


Ametaja baadhi yao kuwa ni mwanadamu anayemiliki hoteli nyingi zaidi duniani, mwingine ni mwanadamu anayemiliki meli nyingi za kifahari kuliko wote Duniani, lakini pia mtu anayemiliki majumba mengi zaidi ya kuonyesha filamu duniani, na alikutana na mwanadamu ambaye anaongoza Kampuni kubwa zaidi ya utalii duniani


Aidha amesema Rais Samia alikutana na mtu anayeongoza mtandao mkubwa kuliko yote duniani ya mawakala wa utalii pamoja na alikutana na watu ambao wanaongoza baraza kubwa zaidi la utalii duniani

Dkt Abbasi amesema watu wote hao wapo tayari kufika Tanzania na taratibu zikikamilika watafika nchini kwa ajili ya shughuli za utalii

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments