5/02/2022

Dr Mengi Alitupatia Jengo Sasa Hatulipi KODI - Chama cha Wafanya biashara wanawake Tanzania TWCC

 


Chama cha Wafanya biashara wanawake Tanzania TWCC kimesema kimewakuza wafanyabiashara wengi sana wanawake kutokana na mchango wa aliyekuwa mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr Reginald Mengi ikiwemo kuwapatia jengo ambalo hadi sasa ndipo makao makuu ya Chama hicho.Ni miaka mitatu sasa TWCC kupitia Kwa Mkurugenzi Mtendaji wake Mwajuma Hamza wanamwelezea Dr Mengi kama mtu wa mfano wa kuigwa (mentor) aliyetamani kuwaona watanzania hususani wafanyabiashara wanawake wakikua kibiashara.


"Hili jengo Dr Mengi ametupatia Hadi Leo tunafanya kazi hapa na endapo tungekuwa tumepanga gharama zingekuwa juu sana na kupitia hapa wanawake wengi mno wamenufaika. "alisema Mwajuma hamza Mkurugenzi Mtendaji TWCC.


Pamoja na hayo pia wanamzunguza kama mtu aliyewapa kibali wafanyabiashara wanaweza kupitia vyombo vyake vya habari hali iliyowapa kujulikana zaidi kibiashara hivyo kutoka wito Kwa wafanyabiashara kuyaenzi aliyoyasisi.


"Mwenyekiti aliamini katika kuweza,kufikia malengo na kuwajali watu wenye makundi maalumu wakiwemo wahitaji pamoja watu wenye ulemavu."alisema Mwajuma.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger