5/30/2022

DTB FC Yabadilisha Jina, Yamtambulisha Rasmi Msemaji Wao Pamoja na Makao Makuu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


KLABU ya DTB iliyopanda Ligi Kuu ya NBC kwa msimu ujao imebadilishwa jina rasmi na kuwa Singida Big Stars Football Club. Timu hiyo imefanikiwa kupanda daraja baada ya kuwa na msimu mzuri katika Ligi Daraja la Kwanza na sasa inajiandaa kupambana katika ngazi ya Ligi Kuu ya NBC msimu ujao.

Moja ya chachu ya mafanikio ya DTB FC katika Ligi Daraja la Kwanza ni uwekezaji mkubwa iliyofanya timu hiyo ambapo iliweza kusajili baadhi ya nyota waliowahi kucheza Ligi Kuu Bara kama vile Amissi Tambwe na Juma Abdul ambao wote waliweza kuhudumu kwa mafanikio katika klabu ya Yanga


Hussein Masanza Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Singida Big Stars
Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Muhibu Kanu amesema kuwa Makao Makuu yatakuwa mkoani Singida, lakini pia Singida Big Stars imemtambulisha rasmi Hussein Masanza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Habari cha timu hiyo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger