Fahamu Mkasa wa Mwanamuziki Harmonize Kukamatwa nchini Kenya, Kisa Kipo Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



STAA wa muziki wa Bongo Fleva na CEO wa Konde Gang, Harmonize usiku wa kuamkia leo Mei 1, 2022  alikamatwa na polisi kisha kuachiwa huru jijini Nairobi nchini Kenya kwa madai ya kulipwa bila kutokea katika baadhi ya kumbi za starehe kwa ajili ya kutumbuiza.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya Harmonize kwa ushirikiano na mwenyeji wake msanii wa vichekesho, Erick Omondi wa nchini Kenya, walitoa ahadi ya kutumbuiza lakini jambo hilo halikufanyika.

Baada ya madai hayo, aliyekua Gavana wa Nairobi, Mike Sonko ambaye alimualika pia Harmonize kutumbuiza mjini Mombasa alisema kuwa Harmonize ameachiwa, na sasa anaelekea Mombasa.

‘”Kuna klabu alitakiwa kutumbuiza lakini hakwenda, sio yeye aliyesaini mkataba bali ni madalali, na sasa yupo huru na anaelekea Mombasa kutumbuiza mashabiki wa Mombasa,’’ anasema Sonko.


Katika ukurasa wa mchekeshaji Erick Omondi, anadai kuwa alifika mapema leo katika Kituo cha Polisi cha Kileleshwa jijini Nairobi ili kumuwekea dhamana Harmonize lakini aliishia kupigwa ngumi ya uso na msanii huyo.

Kwa madai ya Omondi alimshauri Harmonize arudishe pesa kwa wamiliki wa kumbi za starehe lakini Harmonize alikataa.

Baadhi ya wamiliki wa kumbi za starehe wanatupa lawama kwa Harmonize pamoja na Erick Omondi.

“Timu yote wanatakiwa kulaumiwa, Harmonize na Omondi, tumelipia pesa lakini hatujapata huduma, mimi pamoja na mashabiki, na mkataba unasema anatakiwa kutumbuiza kwa saa moja na nusu, lakini hilo halikutokea’,’ anasema mkurugenzi wa kumbi ya starehe ya Captain Lounge.

Kwa upande wa meneja wa Harmonize anayejulikana kama Mchopa, anasema hajapata taarifa za kukamatwa kwake ila anawatafuta Harmonize na timu yake walioko nchini Kenya lakini hawapatikani.’’

“Inawezekana wapo kwenye ndege ndiyo mana hawapatikani,’’ anasema Mchopa.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad