5/03/2022

Fahyma Endeleza Misemo Mtandaoni Baada ya Kufanikisha Kumrudisha Rayvanny Katika Imaya Yake


FAIMA Msangi almaarufu Fahyma au Fahyvanny; ni baby mama wa staa mkubwa wa muziki wa kimataifa wa Tanzania, Rayvanny ambaye kwa sasa anatamba tu na ameanza kunenepa baada ya kufanikiwa kumrejesha jamaa huyo kwenye himaya yake.

Fahyma alitengana na Rayvanny au Chui kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu baada ya kutuhumiana kwa usaliti ambapo jamaa huyo aliangukia kwenye penzi la Paula Kajala; binti wa mwigizaji Kajala Masanja.

Hata hivyo, kuna tetesi kwamba wanga wameshapita na penzi la Rayvanny na Paula.

Sasa; timu ya mwanamama Fahyma ambaye pia ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, wana shangwe na kupiga vigelegele baada ya kitu waliochokipigania kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kimekaa sawa.

Fahyma sasa anatamba kwamba hatimaye amefanikiwa kulirudisha penzi lake na Rayvanny ambaye amezaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Jaydanny.

Fahyma au Fahyvanny.

Kinachoendelea kwa sasa kwa Fahyma ni kushangilia tu na kufanya sherehe huku baadhi ya watu wakisema ameanza kunenepa baada ya kutoka kwenye msongo wa mawazo na kujihakikishia ndiye mama mjengo.

Kupitia Insta Story yake huku akisikiliza Wimbo wa Mama la Mama wa Rayvanny aliomshirikisha Mr Bule, Fahyma anasema; “Aaa…weee mama la mama sina mwingine zaidi yako…”

Kufuatia ishu hiyo, timu yake wameendelea kumpongeza mno Fahyma kwa hatua aliyofikia huku wakimsisitiza kufunga ndoa na Rayvanny moja kwa moja ili ieleweke kabisa kwamba ni wanandoa na kama kuna mwanamke atakuwa anamtaka jamaa huyo basi ajue ni mume wa mtu wa ndoa kabisa.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger