Fainal ya UEFA Baina ya Timu ya Real Madrid na Liverpool Itaoneshw LIVE Kwenye Daraja Jipya la Tanzanite

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 

Daraja Jipya la Tanzanite

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa amesema, kilele cha mashindano ya 67 ya UEFA baina ya Timu ya Real Madrid na Liverpool yataoneshwa mubashara nchini kwenye daraja jipya la Tanzanite jijini Dar es Salaam.


Waziri Mchengerwa amesema mbali na kurusha mubashara mechi hiyo yenye mvuto mkubwa hapa nchini na duniani kote, pia Filamu ya Royal Tour itaoneshwa kabla ya kuanza kwa mechi hiyo ambapo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushuhudia tukio hilo la kihistoria.


Aidha, amesema dhamira ya Serikali kwa sasa ni kuendelea kutumia sekta za michezo na Sanaa kuitangaza Tanzania na vivutio vyake duniani, kwa kuwa zimebeba idadi kubwa ya Tanzania na kuongeza kuwa sekta hizo ndiyo nguvu shawishi ya Serikali zinazowapa watanzania wengi zaidi furaha na faraja.


“Nipende kumpongeza Rais wetu kwa kazi kubwa sana na mikakati thabiti anayoifanya hivi sasa, ya kuifungua Tanzania kupitia sanaa na michezo ambapo hivi karibuni ameandika historia kwa kushiriki moja kwa moja katika kuandaa filamu ya Royal Tour” ameongeza Mchengerwa.


Ametaja baadhi ya mikakati mingine inayofanywa na Rais wa Muungano Samia Suluhu Hassan, kuifungua na kuitangaza Tanzania duniani kupitia Sanaa na michezo kuwa ni pamoja na kuandaa mashindano makubwa barani Afrika ya tuzo za wasanii ili yafanyike hapa nchini yanayojulikana kama MTV Afrika Awards hapo mwakani.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad