5/02/2022

Fisi Tena Bariadi, Mtoto Mwingine Ashambuliwa na Kujeruhiwa Vibaya

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPAMatukio ya Fisi kushambulia watoto na kuwajeruhi vibaya maeneo ya usoni na kichwani yamezidi kushamili katika mji wa Bariadi, ambapo mapema asubuhi ya leo mtoto mwingine jina ni Gindu Kululu (06) mkazi wa mtaa wa Iyoma kata ya Somanda Halmashauri ya Mji wa Bariadi ameshambuliwa na myama huyo.


Wazazi wa mtoto huyo wanaeleza kuwa majira ya Saa 8:00 kamili Asubuhi nyumbani mtoto huyo akiwa na mdogo wake nje, gafla alivamiwa na fisi huyo ambaye alitokea vichaka vilivyopo karibu na nyumbani.


Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mji wa Bariadi Emmanuel Costantine amethibitisha kupokelewa kwa mtoto huyo na hali yake ilivyo.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger