Binti Ampeleka Baba Mkwe Mahakamani Kwa kumzuia Kuolewa na Mpenzi Wake

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPAHalima Yunusa amempeleka baba mkwe katika Mahakama ya Kiislamu Islamic (Sharia Court) katika jimbo la Kaduna nchini Nigeria kwa madai ya kukataa aolewe na mpenzi wake Bashir Yusuf.

Taarifa iliyochapishwa na gazeti la The Daily Trust nchini Nigeria limeripoti kwamba Bi Halima aliiambia mahakama kuwa amependana na mpenzi wake Yusuf , lakini baba yake Yusuf amekataa asimuoe.

Baba yake , Ibrahim, aliiambia mahakama kwamba alikuwa anafahamu kuhusu mapenzi baina ya binti yake na Yusuf, lakini alikuwa hajatimiza vigezo vya kuoa.

Baba huyo alidai kuwa alimwambia mchumba wa binti yake kwamba alikuwa amemtuma awalete wazazi wake lakini hakurudi tena kwa takriban mwaka mmoja.


 
Alijitokeza baaada ya mwaka mmoja baadaye na akamchukua binti yake na wakapotea kwa siku tatu bila kurudi nyumbani ambapo baadaye waliambiwa kuwa walikuwa wameenda kwa shangazi yao, mzee Ibrahim aliiambia mahakama.

Alisema kuwa baadaye walipelekwa katika kituo cha polisi ambako walikamatwa na kupatikana na hatia na baadaye wakaachiliwa kutoka kwenye kituo cha polisi na kutoroka haddi katika mji wa Abuja.

baba yake msichana alisema kuwa baadaye alikutana na baba yake Yusuf ambaye alimuonya kuwa hatamruhusu Yusuf amuoe binti yake.


Baada ya kusikia hoja zao, jaji alimuamrisha baba yake Yusuf kumruhusu kijana wake amuoe Halima na iwapo hatofanya hivyo hmahakama itawafungisha ndoa.

Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad