5/07/2022

Geita ya moto, Mpole hakamatiki Ligi Kuu
Klabu ya soka ya Geita Gold imefanikiwa kutinga tatu bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara kufuatia matokeo ya ushindi wa bao 1-0 walioupata dhidi ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera.
Geita Gold inayoshiriki Ligi Kuu ya Tanzania bara kwa mara ya kwanza kwenye historia yao walipata bao hilo pekee na la ushindi lililofungwa na George Mpole ambaye amefikisha bao la 12 na kuwa kinara wa kufumania nyavu sawa na nyota wa Yanga ,Fiston Mayele.

Chini ya Kocha, Fredy Felix Minziro, Geita Gold imejipambanua kwa kufanya vyema katika mechi zake huku ikionyesha upinzani mkubwa dhidi ya vigogo Simba na Yanga katika mechi zake.

Mwanzoni mwa msimu timu hiyo iliyokuwa inanolewa na Kocha, Etiene Ndayiragije ilikuwa na mwenendo mbaya kiasi cha kuhatarisha uwepo wao kwenye Ligi msimu ujao, ndipo Uongozi wa wachimba madini hao walipoamua kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi pamoja na usajili wa wachezaji wenye uzoefu na Ligi akiwemo beki Kelvin Yondana na Juma Nyoso.

Kwa mwenendo huu upo uwezekano wa Geita Gold kumaliza ndani ya timu nne bora na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa kama ilivyokuwa kwa Biashara Mara United.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger