Gigy Money Amekuja na JIPYA "Tayari Mimi Nimeolewa"


Mwimbaji wa muziki nchini, msanii Gift Stanford maarufu Gigy Money amefunguka kuwa ameshaolewa na mpenzi wake, huku akisisitiza sio kila jambo katika maisha yake la kutangaza.

Kauli hiyo ya Gigy inakuja mara baada ya shabiki mmoja kumtaka kutomkutanisha binti yake, Mayra na kila mwanaume anayekuwa naye katika mahusiano.

"Haina haja ya kumkutanisha binti yako kwa kila mwanaume unaekuwa nae", aliandika Shabiki. Gigy alimjibu kwa kumwambia, "Tumeoana mpendwa, sio lazima kila kitu nitangaze".

Ikumbukwe, Mayra ni binti wa Gigy Money na mtangazaji wa Clouds Fm, Mo Jay.

✍️: @omaryramsey

#SNSEnt
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad