5/09/2022

Gigy Money "Najijua Nina Mdomo Mchafu Sipo Tayari Kuongea"GIFT Stanford almaarufu Gigy Money; ni mwanamama anayejipatia mkate wa siku kupitia Bongo Fleva ambaye anasema kuwa, anajiua ana mdomo mchafu ndiyo maana hayupo tayari kuzungumzia chochote kinachoendelea mitandaoni kati yake na mzazi mwenzake, Mourad Alpha au Mo J.

Akichezesha taya na IJUMAA SHOWBIZ, Gigy ambaye bado anakimbiza na ngoma yake ya Sasambua anasema kuwa, kwa sasa amebadilika tofauti na jinsi watu wanavyomchukulia hivyo hayupo tayari kumzungumzia mtu ambaye siyo sehemu ya maisha yake tena.

“Ninajijua nina mdomo mchafu ndiyo maana sitaki kuzungumza chochote kuhusu huyo mtu (Mo J), halafu Gigy wa sasa siyo kama yule wa zamani, nimebadilika, nahitaji kumlea mwanangu (Mayra) vizuri bila kiki zisizokuwa na maana kwa hiyo naombeni mniache na maisha yangu,” anasema Gigy.

Hivi karibuni uliibuka mtafaruku mkubwa baada ya Mo J kutoa ya moyoni kuwa anaumia kuona baby mama wake huyo anaongea hadharani kuwa yeye hamuhudumii mtoto wao, jambo ambalo anasema siyo kweli hivyo yeye kama mwanaume anahitaji kumchukua mwanaye, Mayra ili amlee mwenyewe kwa sababu mazingira anayoishi ni hatarishi.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger