5/05/2022

Gwajima "Nimeambiwa Baada ya Kujeruhiwa Walichukuliwa na Noah nyeusi"Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima amesema katika mahojiano yake na majeruhi wa Panya Road amemueleza kuwa baada ya tukio vijana hao walichukuliwa na gari mbili nyeusi aina ya Noah


Gwajima amehoji mmiliki wa magari hayo huku akitaka Jeshi la Polisi kufanyia kazi suala hili kwa kuwa inaonekana kuna mtu anawafadhili vijana hao

"Wakati nawahoji hawa waliojeruhiwa, nimezungumza na mmoja ambaye ni dereva maloro anasema baada ya tukio kufanyika hawa vijana walichukuliwa na Noah mbili nyeusi, sasa swali langu ni kwamba Noah ilikuwa ya nani? kwa sababu baada ya tukio hilo likatokea lingine Mbweni, Polisi wafanye kazi inawezekana kuna mtu anawafadhili hawa vijana kwa lengo la kuharibu image ya serikali" - Josephat Gwajima, Mbunge wa Kawe

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger