5/23/2022

H Baba Afunguka Tena Kuhusu Kudhulumiwa na Harmonize "Haya Yote Yatakurudia Utadhulumiwa na Wewe"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwanamuziki aliyewahi kutamba na nyimbo kadhaa ukiwemo wa 'Mpenzi Bubu', Hamisi Baba aka H.Baba kuhusu madai yake amesema anamuachia Mungu pekee na kwasasa amerudi kwenye maisha yake ambayo hadhulumiwi.


H.Baba amefunguka hayo kufuatia madai yake aliyoweka wazi kudai mwanzoni mwa mwezi huu kwa mwanamuziki mwenzake Harmonize ambae wamewahi kufanya nae kazi ya ushirikiano kupitia wimbo wa "Attitude" ambao ulitoka Aprili 23, mwaka jana akiwemo pia gwiji kutokea DR Congo, Awilo Longomba.


H.Baba alidai kudhulumiwa jasho lake (haki) kutokana na ushiriki wake katika wimbo huo kwa kutoambulia chochote katika pande zote mbili yaani audio na video na kusihi kwamba Harmonize amlipe.


Kwenye posti yake hii mpya Instagram, H.Baba ameandika, "Kila chenye mwanzo kina mwisho mdogo wangu, haya yote yatakurudia tu, utadhulumika na wewe na utalalamika kama ulivyolalamika pale Airport, ila jasho langu mimi Mungu atanilipia" - Ameandika H.Baba.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger