5/08/2022

Hali ya DC Korogwe Basilla Mwanukuzi yaimarika Baada ya AjaliMkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Basilla Mwanukuzi amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga, Bombo baada ya kupata ajali ya gari.

Akithibitisha Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, David Mwasimbo amesema ajali imetokea usiku wa kuamkia leo Mei 08, 2022 eneo la Hale lililopo Korogwe katika Barabara ya Tanga-Segera.

“Mkuu wa Wilaya anaendelea vizuri isipokuwa dereva wake hali si nzuri, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, dereva alikuwa anajaribu kuyapita magari mengine na ndipo ajali ikatokea,”amesema Kaimu Kamanda huyo.

Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo, Dkt. Jonathan Gudemo amekiri kuwapokea majeruhi watatu wa ajali hiyo akiwemo mkuu huyo wa wilaya.

Dkt.Gudemo amesema, majeruhi wawili hali zao zinaendelea kuimarika akiwemo Mkuu wa Wilaya na bado wapo chini ya uangalizi wa matabibu

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger