Hatimaye ‘Range’ ya Kajala yaingia TanzaniaHarmonize amemnunulia Gari aina ya Range Rover mpenzi wake wa zamani,mwigizaji kutoka kwenye tasnia ya filamu Tanzania Frida Kajala ikiwa ni sehemu ya kumuomba msamaha lengo kuu likiwa ni kumaliza mgogoro baina yao na kurejesha mahusiano yao kama ilivyokuwa hapo awali.

Mapema Jumatano ya leo Mei 4, 2022, Konde Boy ametuma video kwenye ukurasa wake wa Instagram ikilionyesha gari hilo aina Range Rover nyeupe likiwa na kibao cha namba chenye jina la Kajala huku ikiambatana na ujumbe wa uthibitisho kuwa gari hilo ni kwaajili ya mrembo huyo na kwamba tayari ameagiza gari lingine aina ya Range Rover nyeusi kwa ajili ya mwanamke huyo ampendaye.

Nyota huyo mmiliki wa rekodi kadhaa zinazofanya vizuri, anaeleza kuwa endapo atarudiana na Kajala mpango wake ni kutaka mwanamke wake awe na magari mawili ya kifahari.

“Kajala namba 2 muda huu unaposoma ipo boda Tunduma you can see how Tanzania inavyopepea, waiting for clearance. I’m going to pay taxes tomorrow working day and register. Ready for the boss. Two Range Rovers for the queen,” ameandika Harmonize.


 
Aidha amewatupia kijembe wakosoaji ambao wamekuwa wakimshutumu kwamba hana fedha za kutosha kununua magari ya kifahari na kuwa maneno yake si ya kweli bali ni mwenye kutafuta kiki ili kuendelea kuzungumzwa.

“Mmakonde atapata wapi hela ya kukununulia Range Rover, anatafuta Kiki huyo anatafuta kuzungumziwa, waambie Kajala namba 2 inafika siku ya Ijumaa, Nyeusi kutoka Afrika Kusini.

Kwa hiyo anakwenda kuwa na Range Rover mbili, na mimi nina Vx mbili, nyeupe na nyeusi so na yeye ataenda kuwa na mbili pia. nataka kukufanya wathamani mpaka waanze kukuita Boss Lady,” ameongeza Konde Boy.

Huu ni muendelezo, ikumbukwe Aprili 4 Harmonize ashiriki video ikionyesha gari hilo likiwa na jina la Kajala, na kuambatanisha na ujumbe kuwa gari hilo liko njiani kutoka nchini Afrika ya Kusini linakuja nchini kwa ajili ya mrembo huyo akimtaka amsamehe na kurudi kama walivyokuwa hapo awali.

Na katika kuomba kwake radhi, Konde Boy alikiri wazi makosa yake yote, akisisitiza kwamba anafahamu kuwa alimuumiza Kajala na familia yake, lakini sasa anajutia yaliyotokea.

Taarifa ya Harmonize kununua gari aina ya Range Rover ilikuja wiki moja baada ya msanii huyo kutoa pesa kiasi kinachodaiwa kufika Tsh Milioni 12 kwaajili ya kulipia bango kubwa la matangazo lililokuwa napicha yake na mrembo huyo akimsihi warudiane.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad