Ticker

6/recent/ticker-posts

‘Huddah The Boss’ Aangukia Mapenzini Kwa Mwanariadha Omanyala

 


Mwanariadha Ferdinand Omanyala amekataa vishawishi vya kimapenzi ambavyo sosholaiti Hudda Munroe amekua akivitaja kuwa anamuangukia yeye.


Omanyala amesema kamwe hana haja naye kwenye mahojiano ya simu na Milele FM ya Kenya ambapo alishikilia msimamo kuwa hamna mbinu ambayo sosholaiti huyo maarufu anaweza kutumia kumfikia.


Mtangazaji aliyekuwa akimhoji alimuuliza iwapo amesikia kwamba Huddah anamtamani naye akaangua kicheko kwa sauti akisema “Shetani ashindwe. Huyo hawezi kunipata hata atumie mbinu ipi. Hakuna shida, anachoweza kupata ni kiki tu kwa kutumia jina langu,” alisema.


Young Africans yaitangazia vita Mbeya Kwanza FC

Alishikilia msimamo wake akidokeza kwamba alifunga ukurasa na mambo ya wanawake baada ya kumpata barafu wake wa moyo na Maoni yake yalishirikiwa kwenye ukurasa wa Instagram wa Nairobi Gossip ambao uliwaacha Wakenya mitandaoni wakimsifu kwa kumheshimu mkewe na kutonaswa na mtego wa Huddah


“Kwa kawaida tunajua majivuno ya Huddah hayawezi kumruhusu kuchapisha kitu ambacho hakitatimia.” waliandika baadhi ya wanamitandao huku wengise wkihifu namna amemheshimisha mke wake na wengine wakidai amefata pesa za Riadha.


Katika ripoti tofauti, Omanyala na mpenzi wake Laventa mwenye umri wa miaka 25 wamekuwa pamoja kwa miaka mitano.


Jogoo wa wizi akataa kuuzwa

Mwanariadha huyo alikiri jinsi anavyomepnda barafu wake wa moyo na alihusisha mafanikio yake kwake, akisema mara kwa mara yeye humtia moyo kujisukuma.


Baba huyo wa mtoto mmoja aliahidi kumpiga jeki Laventa, ambaye pia ni mwanariadha ili kufikia ndoto zake akitumai kuwa mwanao wa miaka miwili atafuata nyayo zao.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments