5/08/2022

Huenda Sasa Ndoa ya Will Smith na JADA Pinket Ikafika Mwisho...Waanza Kufanya Mchakato wa Talaka


Ndoto za wanandoa wengi wanapooana huwa ni kuishi pamoja hadi kifo kinapowatenganisha. Vivyo hivyo, wazazi wao, ndugu na jamaa hupenda kushuhudia wanandoa hao wakifanikiwa katika safari ya maisha yao ikiwamo kuwa na familia imara yenye watoto wenye afya bora.


Hata hivyo, siyo wanandoa wote hutimiza ndoto hizo. Baada ya miaka 25 yakuwa pamoja waigizaji Will Smith na Jada Pinkett wamegonga vichwa vya habari, wakihusihswa kuwa wanapanga kutalikiana.


Taarifa ambazo hazijathibitishwa zinaashiria kwamba wawili hao wanajipanga kuanza taratibu za talaka mahakamani ili waweze kugawana mali wanazomiliki kwa pamoja.


Taarifa za wanandoa hao kuachana zinatajwa kuaanzia kwenye mitandao ya kijamii hata kabla ya utani wa Chris Rock kwenye tuzo za Oscar baada ya Jada kukiri kwamba aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine akiwa kwenye ndoa na Will Smith.


Jada na Will walifunga ndoa mwaka 1997, Jada akiwa na ujauzito wa miezi miwili wa mtoto wao wa kwanza Jaden Smith.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger