5/21/2022

Q Chief "Nimeoteshwa Kuwa Mimi Natakiwa Kuwa Mganga"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Ikiwa ni takribani miaka miwili bila kuachia kazi mpya, Q Chief afunguka kurudi kivingine mwezi huu kwa kuachia wimbo mpya ambao una video yake tayari.

Akizungumza kwenye Chill na Sky hapa SnS, Q Chief ameeleza hayo sambamba na kuweka wazi kwa mara ya kwanza kuwa alioteshwa na kupewa mamlaka ya kutibu watu, karama ambayo anasema alikuwa ameandaliwa kuwa nayo tangu zamani na kwasasa yeye ni Sharif.

Akimjibu Sky kuhusiana na masuala ya kuwa Sharif, Q Chief amesema, "Mimi kitaaluma sio mwanamuziki kwa sababu muziki tu naupenda na kiuhalisia kabisa mimi kazi yangu inahitaji utulivu, kazi yangu mimi haionekani lakini mimi naiona" ameeleza Q Chief na kuongeza, "Hicho ndicho kilichokuwa kina nisumbua muda mrefu sana" - Q Chief akiiambia SnS.

Sambamba na hilo Q Chief ameeleza chanzo cha vita na ndugu zake upande wa baba, vita ambayo aliwahi kuisimulia A-Z katika ukurasa wake wa Instagram.

"Mimi nilikuwa napigana vita ya ndani, vita ambayo ni ngumu sana kwa mwanadamu kuishinda na wengi wameishindwa kwa sababu hujui unapigana na nani. Kuna watu walifunga nafsi yangu, tena kuifunga moja kwa moja, na adui mkubwa wa maisha ni ndugu".

"Nilikuja kugundua tunachopigania na ndugu upande wa Baba ni nguvu na mamlaka na kubwa cha ziada ni karama niliyonayo, ndugu wanahoji kwanini nipewe Karama".

"Nimeamua kuzungumza kwakuwa wanaoumia ni watoto wangu sio mashabiki kwa sababu hawajui nini kinachoendelea juu yangu. Kwa sasa kazi nazifanya kwa mikono yangu yaani najua mimi nifanye sayansi gani kwako ili mambo yako yaende" 
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger