Inonga Agawa Tuzo yake kwa Mashabiki

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mlinzi wa kati Henock Inonga, ameamua kugawa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month) kwa mashabiki kutokana na sapoti kubwa wanayompa.
Inonga amekabidhiwa tuzo hiyo na wadhamini Emirate Aluminium ACP ambapo pamoja na kuwashukuru wachezaji wenzake lakini pia ameweka wazi anaitoa kwa mashabiki.

“Hili ni jambo kubwa kwangu, inaniongezea morali kuendelea kuipambania timu. Nawashukuru Emirate Aluminium ACP kwa tuzo hii, nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikiano walionipa lakini naitoa kwa mashabiki,” amesema Inonga.

Kwa upande wake Afisa mahusiano wa Emirate Aluminium, Issa Maeda amesema Inonga amekuwa kwenye kiwango bora na kila mtu ameona kutokana na kiwango alichoonyesha.

Aidha, Maeda amesema kwa sasa wameshusha bei za bidhaa zao zote ili kuwafanya Watanzania wanaotaka kujenga kununua katika kipindi ambacho gharama za maisha zimezidi kupanda.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad