5/01/2022

Kapombe, Inonga, Onyango Mikononi mwa Mashabiki Simba SC

 


Siku moja baada ya kumalizana na Young Africans kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuambulia matokeo ya 0-0, Klabu ya Simba SC imetangaza Wachezaji wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa klabu hiyo.


Simba SC imetangaza orodha hiyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo Mashabiki na Wanachama watapata fursa ya kupiga kura kwa njia ya mtandao na baadae mshindi atatangazwa.


Wachezaji waliotajwa kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki mwezi Aprili ni Beki wa Kulia Shomari Kapombe (Tanzania), Beki wa Kati Inonga Henock (DR Congo) na Beki mwingine wa Kati Joash Onyango (Kenya).


Wachezaji hao watatu wametajwa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kuonyesha uwezo mkubwa katika michezo ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikishio Barani Afrika kwa mwezi April.


Kapombe alikuwa kinara wa kuipa matokeo Simba SC kwenye mchezo wa Mkondo wa Kwanza Hatua ya Robo Fainali Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates, huku akicheza kwa kiwango cha hali ya juu mchezo wa Mkondo wa Pili uliopigwa Afrika Kusini.


Henock Inonga naye alikuwa msaada mkubwa wa Simba SC katika safu ya ulinzi kwenye michezo hiyo ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, huku Onyango aliyekosa mchezo wa mkondo wa kwanza kufuatia adhabu ya kadi tatu za njano akikiwasha barabara Afrika Kusini.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger