Kiba: Bila Uongo Mapenzi Hayaendi, Sijawahi Kuimba Wimbo Wenye Uongo

KING Kiba; ni mfalme wa muziki nchini Tanzania ambaye amezua mjadala kama wote, baada ya kutoa kauli tata kuwa, bila uongo hakuna mapenzi.

King Kiba anasema kuwa, hajawahi kuimba uongo mwingi kama alivyofanya kwenye wimbo mpya wa Niamini alioshirikishwa na msanii Hamadai ambao unaendelea kutikisa kwenye majukwaa ya muziki ndani na nje ya Bongo.

C.E.O huyo wa Lebo ya Kings Music anasema; “Sijawahi kuimba wimbo wenye uongo mwingi kama huu aisee, ila bila uongo pia mapenzi hayaendi vizuri. That’s why nilimuomba Hamadai tufanye hii kwa sababu namkubali sana na wimbo ni mzuri sana, pia Producer Aloneym katisha sana…”

Kauli hiyo ya imesababisha mgawanyiko kwa wafuasi wake ambapo wapo wanaosema ni kweli kwamba, bila uongo mapenzi, lakini wapo wanaosema uongo ni sumu ya mapenzi.

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad