5/19/2022

Kibanda Awakosoa Chadema "Kina Mdee Wamepewa Hukumu ya KIFO, Chadema Wamekosea"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwanahabari na Mchambuzi wa Siasa, Absalom Kibanda amekosoa maamuzi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwafukuza uanachama Halima Mdee na wenzake 18


Amesema "Ni kweli Mdee na wenzake 18 walikosea. Msingi wa makosa yao ni kupinga ubabe wa kihistoria wa Viongozi wenzao na kudai kwao haki kibabe. Ni kweli pia viongozi wakuu CHADEMA waliwahukumu kabla ya vikao. Kosa la kimaadili limetolewa hukumu ya kifo"


Kibanda anaongeza "Huu ni ulaji wa kisiasa. CHADEMA inadai haki yake, akina Mdee wanapigania jasho lao. Orodha inaongezeka, hawakuanza na David Kafulila, Zitto Kabwe, Wilbroad Slaa wala Kitila Mkumbo na hawatamaliza na hawa Wanawake 19. Ukishakula nyama ya mtu huachi"


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger