5/05/2022

Kiingilio Ufunguzi Kombe la Dunia Sh Mil.1.4SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesema limeanza kupokea maombi ya tiketi kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar mwishoni mwa mwaka huu.

Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo amesema tiketi hizo ni kwa ajili ya hatua ya makundi, 16 Bora na Robo Fainali, kwani tiketi za hatua ya Nusu Fainali na Fainali tayari zimekwisha.

“Hata hivyo kwa wale ambao bado wanahitaji tiketi za Nusu Fainali na Fainali waombe moja kwa moja kupitia mtandao wa Fifa,” amesema Ndimbo.

Amesema bei ya tiketi kwa mechi ya ufunguzi kategori 1 itakuwa Qatar riyal 2,250, ambapo kwa mujibu wa maduka ya kubadilishia fedha za kigeni leo Mei 5, 2022, riyal moja ya Qatar ni sawa na Sh 638.56 za Tanzania, hivyo kwa kiingilio cha Qatar riyal 2,250 kwa mechi ya ufunguzi kategori 1 itakuwa sawa na Sh. 1,436,761.67 za Tanzania.


Taarifa inasema kwa kategori 2 itakuwa riyal 1600 (Sh 1,021,697.19) na kategori 3 ni riyal 1100 (Sh 702,416.82).

“Hatua ya makundi kategori 1 ni Qatar riyal 800 (Sh 510,848.59), kategori 2 Qatar riyal 600 (Sh 383,136.45) na kategori 3 Qatar riyal 250 (Sh.159,640.19),” amesema Ndimbo.

Amefafanua kuwa hatua ya 16 bora kategori 1 ni riyal 1000 (Sh 638,560.74), kategori 2 riyal 750 (Sh 478,920.56) na kategori 3 riyal 350 (Sh 223,496.26).


Amesema kwenye Robo Fainali Kategori 1 ni riyal 1550, kategori 2 ni riyal 1050 na kategori 3 ni riyal 750 na kwamba mwisho wa kupokea maombi ni Mei 12 mwaka huu.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger