5/19/2022

Kilichompeleka Mwanamuziki Kendrick Lamar Ghana

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Kundi kubwa la raia wa nchini Ghana hasa wafuatiliaji na wadau wa muziki walipatwa na mshtuko baada ya kuenea kwa habari za ziara ya mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Kendrick Lamar, nchini humo.

Habari zilizoenea kwenye machapisho ya mitandao na vyombo mbali mbali vya habari, hii ilikuwa mara tu, baada ya kuachiwa kwa ‘cover’ ya albamu yake mpya, ‘Mr Morale And The Big Steppers’.

Swali lililokuwa midomoni mwa Waghana wengi lilihusiana na kutaka kujua sababu ya ziara ya rapa huyo mahiri nchini humo, kwani hata baada ya rapa huyo kufika Ghana bado watu wengine hawakuamini uwepo wake hadi picha zilipoanza kusambaa kote mitandaoni.

Ili kuuutaarifu umma ikiwa ni pamoja na kuwaweka wazi wananchi wa Ghana juu ya ziara ya rapa huyo, Ofisi ya Rais nchini humo imetoa taarifa kuwa rapa Kendrick Lamar yuko nchini humo kwa ajili ya kurekodi makala kwa ajili ya album yake.


Makala hiyo inasemekana kuwa sehemu ya mikakati ya kukuza na kuitangaza zaidi album yake mpya ‘Mr Morale And The Big Steppers’ ambayo aliiachia Mei 13, 2022.

Inaelezwa kuwa Rapa huyo mmiliki halali wa Hit songs kama ‘Poetic Justice’ na nyingine kadhaa, ameichagua nchi ya Ghana kama kituo cha kukamilishia mradi wake huo anaotarajia kuupeleka mbali zaidi.

Ofisi ya masuala ya Diaspora ya Rais wa Ghana imetoa picha za matukio kadhaa ya rapa huyo akiwa katika maeneo tofauti tofauti akitangaza albamu yake mpya.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger