Kocha Pablo Afunguka "Mchezo dhidi ya Namungo mgumu kwetu"Ligi Kuu soka Tanzania bara NBC Premier League inaendela leo kwa mchezo mmoja ambapo klabu ya Namungo FC watakuwa wenyeji wa Saimba SC. Mchezo huu unachezwa Saa 10:00 Jioni uwanja wa Ilulu Mkoani Lindi.

Kuelekea mchezo huu kocha wa Simba Pablo Franco Martin amesema mchezo wa leo utakuwa mgumu kwao kutokana na kukosa muda wa kutosha wa maandalizi kuelekea mchezo huu.

“Nadhani mchezo utakuwa mgumu zaidi kwetu sababu hatujapata muda wa maandalizi. Tumetoka kucheza mechi kubwa ya Derby na hapo hapo tukatakiwa kusafiri kuja huku. Naikumbuka vizuri Namungo katika michuano ya Mapinduzi, tuliwafunga mabao 2-1 lakini mechi ilikuwa ngumu na ushindani mkubwa. Sisi ni Simba tutajitahidi kutafuta alama tatu,” amesema Pablo.

Simba wanaingia kwenye mchezo huu wakiwa wametoka kupata suluhu kwenye mchezo wa Ligi dhidi ya watani zao wa jadi na vinara wa ligi Kuu Yanga SC mchezo uliochezwa Jumamosi Aprili 30, 2022. Ambayo ilikuwa ni suluhu ya pili mfululizo kwenye michezo ya Ligi baada ya ile ya Polisi Tanzania.

Rekodi zinaibeba Simba dhidi ya Namungo kwenye michezo 5 ya Ligi kuu waliokutana Simba wameshinda michezlo 4 na sare mchezo mmoja na mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0. Na msimu uliopijta mchezo uliochezwa mkoani Lindi Simba ilishinda kwa mabao 3-1.


Timu hizi zinatofautiana alama 13 kwenye msimamo wa Ligi, Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na alama 42, katika michezo 20 wakati The Southern Killes wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 29 katika michezo 21
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad