5/31/2022

Kocha Pablo Atimuliwa Simba, Agomea Barua

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


VIKAO vya siku mbili ndani ya Simba vimeamua rasmi kuachana na kocha mkuu Pablo Franco kwa kile kilichodaiwa ni kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
Simba imepoteza mataji yake yote mawili la Ligi Kuu Bara ambalo walilitwaa kwa mara nne mfululizo pamoja na taji la Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) walilobeba mara mbili mfululizo.
Habari za kikao hicho zilinaswa na Mwanaspoti kwamba wamefikia makubaliano hayo na tayari Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez alimwandikia barua ya kuvunja mkataba kocha huyo aliyomtumia jana jioni.
Pablo amekiri kupokea barua hiyo na kwamba alimrudishia bosi wake kwani kuna vitu ndani ya barua hiyo vilikuwa havijakaa sawa hivyo anachosubiri sasa ni Barbara kufanya marekebisho hayo ili asaini.
"Ni kweli tulikuwa na kikao na mabosi wangu na kuna mambo sikukubaliana nayo hususani upande wa usajili, jioni CEO alinitumia barua ya kuvunja mkataba lakini ilikuwa na upungufu hivyo sikusaini nilimrudishia ili arekebishe.
"Sikupanga kuondoka Simba kwani tayari nilikuwa nimeikatia Visa familia yangu ya kuishi hapa kwa mwaka mmoja, hivyo nasubiri akirekebisha hiyo barua na kuyaweka yale niliyoyapendekeza ambayo ni maslahi basi nitasaini kuvunja mkataba," amesema Pablo ambaye aliingia Simba Novemba mwaka jana.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger