5/20/2022

Korea Kaskazini yapambana na Covid kwa maji ya chumvi na tangawizi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Korea Kaskazini inapambana kupunguza maambukizi ya Covid kwa raia wake ambao idadi kubwa hawajachanjwa, bila utumiaji wa dawa bora za kukinga virusi.

Mwanzoni mwa 2020, nchi ilifunga mipaka yake kujaribu kujikinga na janga hili.

Uongozi wake hadi sasa umekataa msaada wa matibabu kutoka nje.

Vyombo vya habari vya serikali vimekuwa vikipendekeza matibabu mbalimbali ya asili ili kukabiliana na kile kinachojulikana kama "homa"

Vinywaji vya moto
Kwa wale ambao si wagonjwa sana, gazeti la chama tawala Rodong Sinmun lilipendekeza tiba za asili ikiwemo tangawizi au chai ya honeysuckle na kinywaji cha majani ya Willow

Vinywaji moto vinaweza kutuliza baadhi ya dalili za Covid, kama vile vidonda vya koo au kikohozi na kusaidia kumuongezea maji wakati wagonjwa wanapopoteza maji mengi kuliko kawaida.

Tangawizi na jani la Willow pia hupunguza kuvimba na maumivu.

Lakini sio matibabu ya virusi yenyewe.

Maji ya chumvi
Vyombo vya habari vya serikali hivi majuzi viliwahoji wanandoa ambao walipendekeza kusukutua na maji ya chumvi asubuhi na usiku.

"Maelfu ya tani za chumvi" zilitumwa Pyongyang kufanya kama"suluhisho la dawa", shirika la habari la serikali liliripoti.

Tafiti zingine zinaonyesha kusukutua na kusafisha pua kwa maji ya chumvi kupambana na virus ambavyo husababisha homa ya kawaida.

Lakini kuna ushahidi mdogo kwamba wanapunguza kuenea kwa Covid.


Kuosha midomo kunaweza kuua virusi kwenye maabara, utafiti uligundua.

Lakini haijaonyesha kusaidia binadamu.

Covid mara nyingi hupatikana kwa kuvuta matone madogo ya maji maji kupitia pua na mdomo, kwa hivyo kusukutua kutashambulia sehemu moja tu ya kuingia.

Na mara tu virusi vinapoingia huenea zaidi ndani ya viungo ambapo hakuna kiasi cha kusukutua kinaweza kufikia.

Dawa za kupunguza maumivu na za vijiuasumu (antibiotics)
Televisheni ya serikali imewashauri wagonjwa kutumia dawa za kutuliza maumivu kama vile ibuprofen na vile vile amoksilini na vijiuasumu vingine.Ibuprofen (na paracetamol) inaweza kupunguza joto na kupunguza dalili kama vile maumivu ya kichwa au koo.

Lakini hawataondoa virusi au kuzuia kutokea.

Antibiotics, iliyokusudiwa kwa maambukizi ya bakteria sio virusi, haipendekezWi.

Na utumiaji wa vijiuasumu huhatarisha kupata wadudu sugu.

Utafiti wa kimaabara unaonyesha kuwa baadhi wanaweza kupunguza kasi ya kuenea kwa baadhi ya virusi, ikiwemo Covid.

Na uchunguzi wa dawa ya azithromycin uligundua kuwa ilileta tofauti kidogo au hakukuwa na tofauti kabisa kwa dalili za Covid, kuna uwezekano wa kulazwa hospitalini au kifo.

Kuna dawa zilizoidhinishwa za kuzuia watu walio na Covid kuishia hospitalini:

dawa za kuzuia virusi paxlovid, molnupiravir na remdesivi

matibabu ya kinga mwili ambayo yanafuata mfumo wa kinga

Lakini ufanisi wa hizi dawa ni tofauti.

Mfumo wa afya
Mfumo wa afya wa Korea Kaskazini umeanzishwa ili kutoa huduma za matibabu bila malipo kuanzia huduma za msingi katika ngazi ya kijiji hadi matibabu maalumu katika hospitali za serikali (kawaida katika vituo vya mijini).

Lakini uchumi umedorora katika miaka ya hivi karibuni kwa sababu ya vikwazo na hali mbaya ya hewa kama vile ukame.

Kufunga mipaka ya nchi na hatua kali za marufuku ya kutotoka nje pia zitakuwa na athari mbaya.


Hasa nje ya Pyongyang, mfumo wa afya unafikiriwa kukabiliwa na uhaba wa wafanyakazi, madawa na vifaa.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa, mwaka jana, ilisema: "Baadhi ya mitambo ya dawa, chanjo na vifaa vya matibabu haifikii kiwango cha utendaji mzuri wa WHO [Shirika la Afya Ulimwenguni] na haikidhi mahitaji ya ndani pia."

Wakosoaji wengi wa Korea Kaskazini waliohamia Korea Kusini wameeleza juu ya kulazimika kulipia dawa au kupata matibabu na dawa pekee kwa wanachama wa chama tawala.

Lakini vyombo vya habari vya serikali vinasema sasa inaongeza uzalishaji.

Msaada wa kimataifa
Korea Kaskazini ilikataa dozi milioni tatu zilizotengenezwa na China, mwaka jana - na inaripotiwa kukataa misaada mingine chini ya Covax, mpango wa kimataifa wa kugawana chanjo.

Korea Kusini inasema nchini hiyo haijajibu ombo lao la kuwapa chanjo, vifaa vya matibabu na wafanyikazi.

Korea Kaskazini imeripotiwa hivi karibuni kutuma mipango mitatu ya kukusanya vifaa vya matibabu kutoka Shenyang.

Hizi hazikujumuisha "vifaa vya kukabiliana na janga", wizara ya mambo ya nje ya China ilisema, lakini ilikuwa "tayari kufanya kazi na Korea Kaskazini ... katika vita dhidi ya ugonjwa huo".


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger