Kudhalilisha vyama vya Siasa iwe Mwisho

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amewataka viongozi wa vyama vya siasa nchini kuacha tabia ya kurushiana maneno ya matusi na ya kuudhi kwenye mitandao au mikutano ya kisiasa
Mbowe amesema kutofautiana kwa mawazo miongoni mwa vyama vya siasa ndio ukuaji wa Demokrasia na haipaswi kuwa chanzo cha chuki

Kauli hiyo ameitoa katika hotuba yake ya kufungua Mkutano wa Baraza kuu la Chama hicho unaofanyika Dar es salaam

"Chama chetu kinapaswa kuwa wanyenyekevu kwa vyama vingine vya siasa, kuheshimu maamuzi ya vyama vingine vya siasa, na chama hiki kifanye kazi ya kujenga harakati za kweli na sio kazi ya kutukana vyama vingine kwenye mitandao au kwenye mikutano"

"Ninaona kwenye mitandao maneno ya maudhi ambayo viongozi wangu mnafanya kudhalilisha vyama vingine, hii inatakiwa kuisha sasa, tuheshimu Vyama vya wenzetu tuheshimu mawazo yao, tunapotofautiana ndio Demokrasia yenyewe" amesema Mbowe


Aidha Mbowe ameeleza kuwa kutofautiana kwa ajenda baina ya CHADEMA na ACT Wazalendo kunapaswa kuheshimiwa na haina haja ya kuonana wabaya

"Wenzetu wa ACT wamekuwa na ajenda yao ya Tume huru, CHADEMA hatuna haki ya kuwaambia msitake Tume huru, wacha watake wanachotaka wao, tunatofautiana katika njia na hiyo ndio namna ya kujenga Demokrasia, sio kila mmoja anayepingana na CHADEMA basi ni mbaya, hapana" 

"Kwanza niweke sawa, hatukatai tunahitaji Tume huru, kwahiyo ajenda ya ACT ni ajenda yeto wote, lakini Tume huru haipaswi kusimamisha mchakato wa Katiba, mchakato wa Katiba uendelee wakati wengine wanarekebisha sheria ambazo ni mbovu, haya mambo yaende kwa kutegemeana" 


Mbowe amefungua Rasmi mkutano wa Baraza kuu la CHADEMA  ambalo litajadili ajenda mbalimbali za kujenga chama hicho huku ajenda kubwa inayosubiriwa ni maamuzi ya Rufaa ya wabunge 19 wa viti maalum waliofutwa uanachama na kisha kukata rufaa.

CHADEMA inatarajiwa kutoa majibu ya rufaa zao katika mkutano huo 


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad