5/08/2022

Lulu Afunguka Mapya Hakuna Starehe Ambazo Hajapitia, “Maisha ya Ujana Yaacheni”Elizabeth Michael almaarufu Lulu au Mama G; ni staa wa Bongo Movies tangu kitambo hicho akiwa na umri wa miaka mitano hadi leo ni mke na mama ambaye anasema kuwa, hivi sasa ni mtu wa kukaa nyumbani tu kila wakati kwa sababu ukweli ni kwamba hakuna starehe ambazo hajapitia au hakuna sehemu aliyoacha kwenda.

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Lulu ambaye pia ni ni mfanyabiashara wa nguo mbalimbali za kike, anasema kuwa, anachoamini ni kwamba mambo ya zamani ilikuwa ni utoto tu na si kitu kingine.

Lulu ambaye ni mama wa mtoto mmoja na mke wa ndoa wa Majizzo anasema kuwa, hivi sasa amekuwa tofauti kabisa na ukichanganya na kulea, basi vitu vimebadilika kabisa na kikubwa zaidi kwake ni mtoto wake tu na si kitu kingine.

“Jamani naweza kusema maisha ya ujana yaacheni kabisa, yana mambo mengi sana, lakini Mungu ni mwema sana kwani kila kitu kimebadilika kabisa, naweza hata kumaliza miaka miwili bila kujua kabisa hata kumbi yoyote ya starehe, kwanza akili yangu iko kwa mtoto wangu ambaye ndiye amebadilisha kila kitu kwenye maisha yangu,” anasema Lulu ambaye ni mmiliki wa duka kubwa la nguo la Drip By Lizzy lililopo Sinza jijini Dar.


HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger