5/27/2022

Mahakama Nchini Rwanda imemwachia kwa Dhamana Miss Rwanda 2017

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Mahakama nchini Rwanda imemwachia kwa dhamana Miss Rwanda 2017, Elsa Iradukunda, anayekabiliwa na mashtaka ya kutoa ushahidi wa uongo pamoja na kughushi nyaraka.

Kesi hiyo inahusishwa na mwandaaji wa mashindano ya ulimbwende, Dieudonne Ishimwe anayetuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono.

Ishimwe ni kiongozi wa kampuni ya Rwanda Inspiration Backup, inayoandaa mashindano hayo ya urembo ya kila mwaka ya Miss Rwanda.

Fahamu, Miss Rwanda ilianza kushiriki shindano la dunia la Miss World mwaka 2016, kwa mujibu wa tovuti ya kampuni hiyo. Inasifu shindano lake kuwa linaongoza kwa aubora katika nchi za Afrika Mashariki.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger